25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

RC ASIMAMISHA UCHIMBAJI DHAHABU

Na TIGANYA VINCENT,

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesimamisha kwa muda uchimbaji wa dhahabu katika machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge  kuepusha maafa zaidi.

Hatua hiyo inatokana na  maafa yaliyokea hivi karibuni ambako wachimbaji wadogo  sita walifariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi na mmoja  kwa kukosa hewa, wakati wakichimba dhahabu katika eneo hilo.

Uamuzi huo ulitolewa jana wilayani Sikonge na RC Mwanri   kwa kushirikiana na Kamati na Ulinzi na Usalama mkoani humo baada ya  kutembelea machimbo yaliyosababisha maafa hayo   kujionea  na  kuwapa pole wafiwa.

Alisema  yeye na kamati yake waliona ni vema wasimamishe kwa muda ili taratibu zote za kuhakikisha usalama na zile Baraza la Taifa la Mazingira za mpango wa ulinzi wa mazingira  zinafuatwa kabla ya kendelea na shughuli za uchimbaji.

Mwamri  alisema    lengo ni kutaka wachimbaji hao waendelee kuchimba katika hali ya usalama bila kuhatarisha maisha yao na nguvu kazi ya taifa.

Aliwaagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati na Magharibi, Salim Salim na  Ofisa Madini Mkazi wa Tabora, Laurent Mayala kuhakisha  umbali kutoka shimo moja la uchimbaji hadi jingine unazingatia matakwa ya sheria na kanuni kuliko ilivyo sasa ambako kutoka shimo hadi shimo ni mita tatu hali ambayo ni hatari.

Rc alisema ni vema ofisi hizo zikahakikisha  zinawapanga wachimbaji wadogo   hao kulingana na matakwa ya sheria na siyo kuwaacha  ovyo ovyo.

  “Mimi siko tayari kuona watu wengine zaidi wanakufa  kwa sababu ya uchimbaji usiozingatia matakwa ya sheria na ambao hauna baraka za NEMC.

“Hivyo kaeni chini na wamiliki wa mgodi muwapange vizuri kwa kuzingatia sheria na bila upendeleo.

“Serikali ya Awamu ya Tano  ilishaahidi kuwa itawashika mkono wachimbaji wadogo lakini ni vema tukahakikisha  mpango wa ulinzi wa  mazingira umezingatiwa.

“Pia wawepo wakaguzi watakaohakikisha  taratibu za umbali kutoka shimo hadi shimo umezingatiwa kulinda usalama wao kwanza,” alisema.

Aliwaagiza maofisa madini kuharakisha kufuatilia  kibali cha NEMC na kuandaa mpango kazi wa uchimbaji mzuri na salama  vijana wanaojihusisha na uchimbaji wa madini   Kitunda wasikae muda mrefu bila kuendelea na kazi yao ya uchimbaji madini.

Eneo la machimbo ya Kitunda lina wachimbaji zaidi ya 10,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles