29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rc aagiza mkuu wa shule kusimamishwa

Mwandishi wetu -Tabora

UONGOZI wa Mkoa wa Tabora,umemsimamisha kwa muda Mkuu wa Shule ya Sekondari Kamagi wilayani Sikonge, Juma Nkungu kupisha uchunguzi juu ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili, ikiwamo mbao 180 zilizoondolewa bila kufuata utaratibu.

Hatua hiyo, imechukuliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa ziara  ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo na kukuta upungufu mkubwa.

Alisema mapema mwaka huu, alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi ya ujenzi wa bwalo  alikuta mbao 180 ni mbovu ambazo zilikuwa hazifai kwa ujenzi na kuagiza ziondolewe na mzabuni aliyewauzia mao  apeleke nyingine kufidia.

Alisema baada ya kufika mara ya pili ili kuona kama agizo lake limetekelezwa, alipokuta kuna upungufu mwingine,ikiwamo kutokuwepo na ushahidi unaoonyesha kama kweli mbao mbovu zilizopoondewa na zilipelekwa wapi na fidia yake.

“Kukosekana kwa nyaraka zinazoonyesha kutoka na kupokelewa kwa mzigo wa mbao hizo kunatia shaka , jambo linaoonyesha kuwa kuna uwezekano wa mchezo mchafu umefanyika,” alisema.

Aliongeza kuwa hata diwani wa eneo hilo na wajumbe wa kamati zote tatu ya ujenzi, mapokezi na manunuzi walipoulizwa, walisema hawajui siku mbao mbovu zilizopotoka na siku za fidia zilipopokelewa na kuwa mkuu wa shule hiyo ndio pekee anajua.

Kutokana na upungufu huo,alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sikonge (OCD) kuimarisha ulinzi  ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari hiyo ili asiingie ofisini kwa ajili kupisha timu ya ukaguzi.

Alisema wakati uchunguzi ukiendelea, Ofisa Elimu Wilaya ya Sikonge, Yussuf Hamza atafute  mwalimu wa kukaimu nafasi hiyo.

Alisema baada ya uchunguzi wampatie taarifa na kama watakuta hakuna kasoro arudishwe katika nafasi yake.

“Nyie fanyeni uchunguzi endapo mtamkuta hana tatizo , mrudishe katika nafasi yake…mimi sitaki kumuonea mtu …ninachotaka kujua ni thamani halisi ya fedha ya umma iliyotumika kama inalingana na huduma iliyotolewa” alisisitiza.

Naye Hamza alisema kwa muda mrefu aliomba mchangunuo wa matumizi ya fedha za mradi huo, lakini alizungushwa bila kupata mfanikio, ndipo akachukua uamuzi wa kumwita katibu wa ujenzi na kumfungia ofisini kwake ili atoe taarifa na ndipo ilipopatikana na kuonekana na mapungufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles