29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanakijiji 12 mbaroni kwa kufunga barabara

Gurian Adolf-Kalambo

JESHI la Polisi wilayani Kalambo mkoani Rukwa, limewakamata  na kuweka mahabusu kwa muda usiojulikana wakazi 12 wa Kijiji cha Ntatanda kwa tuhuma za kufunga barabara  inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Wananchi wamekamatwa, baada ya kuchimba mashimo na kuweka magogo na kusimika bendera zao katikati ya barabara  na kuzuia msafara wa mkuu wa wilaya hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana na kusababisha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura kushindwa kuendelea na ziara aliyokuwa akiifanya katika vijiji vilivyopo mpakani kwa lengo la kutatua kero mbalimbali.

Akiwa kijijini hapo, alikuta vijana12 wakiwa  na majembe, mapanga na sururu, wameziba barabara kwa kuweka magogo ili kuzuia magari yasipite.

Kutokana na hali hiyo, alilazimika kuliita gari la polisi na kuagiza wakamatwe na kuwafunguilia kesi mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Akizungumza baada ya kusitisha kwa muda msafara wake,Binyura kitendo hicho hakikubaliki kutokana kwani wangeweza  kusababisha ajari.

 ‘Kitendo walichokifanya cha kuzuia barabara kwa kuweka magogo,kitendo kibaya hawa walikuwa na nia mbaya kama  gari lolote lingepita lingeweza kupata kupata ajari, mashimo na magogo haya kweli ndugu zangu mnaweka barabarani,’’alihoji.

Baada ya kukutana na hali hiyo, msafara wake ulilazimika kusitishwa kwa muda  na kuanza kufanya mahojiano na vijana hao.

‘’Tumewakamata wote na watahojiwa, kisha kufikishwa mahakamani ili wakaeleze kwanini  waliamua kufanya kitendo kama hiki, wameishi hapa miaka mingi na hakuna ajali mbaya  ambazo zimewahi kutokea.

“Kama zingekuwa zimetokea wangetoa taarifa  kwa  viongozi husika ili waweze kuweka matuta, lakini kufanya hivi.

Aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kujichululia sheria mikononi,badala  yake watoe taarifa kwa  viongozi wa serikali za vijiji na kata  pindi panapokuwa pametokea tatizo la aina yoyote kwa lengo la kuepukana na matatizo yasiokuwa ya lazima.

‘’Nawaomba wananchi muache tabia ya kujichukulia shera mikononi,  ikiwamo kuchimba barabara  bila kuzingatia athari zinazoweza kutokea,’’alisema Binyura.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, JulisTete alikemea vikali kitendo hicho na kusema hakikubaliki na kuahidi kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara juu  ya athari  za kujichukulia sheria mikononi.

‘Kitendo hiki nakilaani tena kwa nguvu zote,walichofanya wananchi wangu ni uvunjifu wa sheria na hakikubariki hata kidogo’’alisema

Alisema wananchi hao walilazimika kufanya hivyo kwa kile walichodai wamechoshwa kuona mifugo yao, ikiwamo nguruwe na kuku kugongwa na magari mara kwa mara yanayofanya safari zake kutoka Kaseshya kwenda nchini Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles