24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rayvanny anogesha albamu ya Zlatan

NA MWANDISHI WETU

STAA wa Bongo Fleva, Rayvanny, amepata bahati ya kuwa mmoja ya wasanii nyota walioshirikishwa kwenye albamu, Resan ya nguli wa miondoko ya Zanku, Zlatan Ibile kutoka Nigeria.

Mbali na Rayvanny, ndani ya albamu hiyo iliyotoka hivi karibuni ikiwa na ngoma 12 zinazolenga kuelezea safari yake ya muziki, uchapakazi, kujituma na kufurahia maisha kuna mastaa wengine kama vile Davido, Buju, Ms Banks, Sho Madjoz, Rhyno, Flavouur, Bella Shmurda.

Akizungumzia albamu hiyo, Zlatan amesema Resan ni neno la ki Sweden lenye maana ya safari iliyotangazwa rasmi mwishoni mwa ziara yake Uingereza na kuzua gumzo ndani ya O2 Academy.

Albamu hiyo iliyopokewa kwa kishindo na mashabiki imetengenezwa na watayarishaji wakubwa kama P.Prime, Niphkeys, Solshine, Spellz, Yung Willis, Rexxie, Steph, T-Keys na  Czech.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles