25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Raptors wakaribia kuandika historia NBA

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya  mpira wa kikapu ya Toronto Raptors imejiweka katika nafasi nzuri ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Marekani maarufu kama NBA, baada yajana kuibuka na ushindi wa vikapu 105-92 dhidi ya Golden State Warriors. 

Kwa ushindi huo, Raptors inaongoza kwa ushindi wa michezo mitatu dhidi ya mmoja wa Worriors, hivyo inahitaji kupataushindi moja tu katika michezo mitatu iliyosalia kati ya timu hizo ili kutwaa ubingwa.

Katika mchezo wa jana, Kawhi Leonard aliwaongoza wachezaji wa Raptors  baada ya kufunga vikapu 36,  huku Serge Ibaka akitokea bench na kufunga vikapu 20.

Wachezaji Pascal Siakam na Kyle Lowry, pia walitoa mchango mkubwa uliosaidia kufanikisha ushindi huo.

Mchezo namba tano kati ya timu hizo utachezwa kesho Alfajiri, Scotiabank Arena, Canada.

Raptors itakuwa ikipata sapoti kubwa ya  kushangiliwa na shabiki wao mkubwa mwanamuziki wa Rap, Drake.

Raptors haijawai kushinda ubingwa wa NBA, hivyo itakua imeandika historia mpya kama itafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi hiyo itakapocheza nyumbani kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles