28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kitisho cha Trump: Mexico yatangaza hatua isiyo ya kawaida kwa wahamiaji haramu

WASHINGTON- Marekani

MEXICO imekubali kuchukua ‘hatua isiyo ya kawaida’ itakayosaidia kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji kwenda Marekani  ili kuepuka vitisho vilivyotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump la ongezeko la ushuru wa bidhaa.

Marekani na Mexico zimekuwa katika mazungumzo kwa siku mbili yaliyomalizika jana juu ya suala hilo la kudhibiti wahamiaji haramu.

Jana kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Trump aliandika maandiko kadhaa, akibainisha kuwa  anasitisha mpango wa kuzuia ongezeko la  ushuru kwa muda usiojulikana baada ya kukubaliana na Mexico juu ya suala hilo la wahamiaji haramu.

Kama njia ya kuishinikiza Mexico kuzuia wimbi kubwa la wahamiaji wake haramu nchini Marekani, Trump alitishia kongeza ushuru wa asilimia tano kila mwezi katika bidhaa za nchi hiyo.

“Ninafurahi kukujulisha kuwa Marekani imefikia makubaliano yaliyosainiwa na Mexico. Ushuru ambao ulipangwa kutekelezwa na Marekani Jumatatu dhidi ya Mexico umesimamishwa kwa muda” lilisomeka andiko la Trump.

Makubaliano hayo ya sasa  pia yalithibishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico,  Marcelo Ebrard,  aliyesema kwamba  yamefikia mwisho baada ya siku mbili za mazungumzo yaliyoshuhudia Marekani  ikihitaji kukomeshwa kwa vitendo vya wahamiaji haramu  Amerika ya Kati.

Maofisa wa nchi hizo mbili walikuwa katika mazungumzo ya wakijadili mwakafa wa kuzuia ongezeko la ushuru wa bidhaa. 

Katika azimio lao la pamoja lililotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani,  nchi hizo mbili zilisema Mexico itachukua hatua kali kudhibiti  wahamiaji haramu na biashara ya binadamu.

Marekani pia imekubali kutanua programu yake ya kuwarudisha wakimbizi Mexico wakati wakisubiri malalamiko yao kupitiwa.

Nchi zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano  ikiwa ni pamoja na kuratibu hatua fulani fulani pamoja na kushirikiana taarifa.

Pia wameazimia majadiliano kuendelea,  na kwamba makubaliano ya mwisho yatatangazwa ndani ya siku 90.

Wastani wa watu milioni moja wanatajwa kupita kila mwaka katika mpaka kati ya Mexico na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles