28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ramaphosa ashutumu mashambulizi dhidi ya wageni

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameshutumu ghasia za hivi karibuni za mashambulizi dhidi ya wageni na kutoa wito kwa taasisi za kiusalama kuwakamata wanaotekeleza vitendo hivyo.

Amesema ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na wengine wa mataifa ya Afrika katika Jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia.

Wiki iliopita, makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao kukimbia waandamanaji

waliotajawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

‘’Leo uchumi wetu na faida za jamii yetu zinatokana biashara na uwekezaji kutoka kwa washirika wetu wa Afrika, wakiwamo wanaoishi hapa, ambapo wana mchango mkubwa wa maendeleo ya taifa hili.

Maendeleo ya Afrika yanatokana na ongezeko la watu na mizigo kutoka eneo moja hadi jingine kati ya mataifa tofauti ili sote tuweze kufaidika.  hatutakubali kuwaruhusu wahalifu kurudisha nyuma hatua zilizopigwa’’.

Kwa mujibu wa Egbert Mkoko, ambaye ni raia wa Tanzania anayeishi katika Jimbo la Kwazulu Natal anasema hali si shwari hususan miongoni mwa raia wa Zimbabwe, Malawi na Ethiopia ambao ndio wengi wanaotafuta maisha eneo hilo.

Mkoko anasema kuna baadhi ya watu wanaodaiwa kuuawa eneo hilo.

‘’Vurugu zilizotokea awali zimeibuka tena na chanzo ni wageni wanaoishi hapa kudaiwa kuchukua ajira za raia wa taifa hilo,” alisema.

Anasema kuwa bado hakuna suluhu yoyote iliotolewa na serikali hatua ambayo imewafanya raia wengi wa kigeni kuamua kusalia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles