25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Wapinzani waongoza miji mikubwa Uturuki

ANKRA, UTURUKI

CHAMA cha Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, The Justice and Development Party (AKP) kinakabiliwa na hatari ya kushindwa katika miji mikubwa ya Ankara na Istanbul.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Juu ya uchaguzi, Sadi Guven, mgombea wa upinzani anaongoza nafasi ya meya wa mji wa Istanbul huku mwingine akiwa tayari ameshinda mjini Ankara.

Lakini Rais Erdogan amewataka wafuasi wake kutosikitikia matokeo hayo.

“Ningependa kuwaomba kubakia kitu kimoja. Msiumizwe au kuvunjwa moyo kwa kusema hamkutarajia matokeo kama haya. Tunacho chama kilichoshinda asilimia 52 ya kura zote.”

“AKP ndiyo mshindi wa uchaguzi huu. Tunachosema ni twende mbele. Ndiyo maana tutafakari juu ya makosa yetu, kuyarekebisha na kuendelea na kazi nyingine,” alisema

Erdogan siku ya Jumapili. Rais Erdogan, ambaye uwezo wake wa kushinda mfululizo katika uchaguzi ni wa kipekee katika historia ya Uturuki, alionekana kudhoofi ka safari hii.

Hilo linatokana na mdororo wa kiuchumi uliolikumba taifa hilo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha

muongo mmoja, ambapo viwango vya ukosefu wa ajira na mfumuko wa beiko juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles