Houston Marekani
Rais 41 zamani wa Marekani George H. W Bush amefariki dunia akiwa na miaka 94.
Msemaji wa fa milia yake Jim McGrathamethibitisha taarifa za kifo chake ambapo amesema Bush amefariki siku ya Ijumaa Novemba 30 mjini Houston miezi nane baada ya kifo cha mke wake Barbara Bush aliyefariki Aprili 2018.
“Jeb, Neil, Marvin, Doro na mimi tunahuzunika kutangaza kwamba baada ya miaka 94 , Baba yetu mpendwa amefariki,” mwanawe, Rais wa zamani Bush, alisema katika taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter na msemaji wa familia Jim.
Bush aliongoza nchi hiyo tangu 1989 -1993 na katika uongozi wake alifanikiwa katika kampeni ya kumuondoa Saddam Hussen Kuwait.
Aidha Bush alikuwa mtu wa sifa za hali ya juu baba bora wa watoto wake wa kiume na wakike.