Karia: Ifikapo Januari viwanja vyote vya mpira vitatumia mfumo wa kieletroniki

0
1176

OSCAR ASSENGA, TANGA


Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema kuwa ifikapo Januari mwakani viwanja vyote nchini vitatumia mfumo wa kieletroniki katika ukataji tiketi za kuingia uwanjani.

Karia amesema hayo leo Desemba 1 alipofungua mkutano wa baraza kuu la TPLB lililofanyika mjini Tanga.

Amesema wataanza mazungumzo na Chama cha Mapinduzi pamoja na Halmashauri mbalimbali zinazomiliki viwanja ambavyo hutumiwa na baadhi ya timu za zinzaoshiriki Ligi kuu bara.

“Labda niwaambie kwamba viwanja vyote hapa nchini ifikapo Januari vitatakiwa kuwa na mashine kwa ajili ya ukataji wa tiketi na zoezi hilo litaanza mazungumzo na halmashauri pamoja na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” amesema Rais Karia.

Karia amesema zoezi hilo litafanyika kama linavyofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Uhuru, Chamazi na Taifa vya jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here