KINSHASA,CONGO DR
WIZARA Mambo ya Nje imesema kwamba Rais Felix Tshisekedi atafanya ziara mjini Washington DC mapema mwezi ujao kujadili kuimarisha uchumi na usalama.
Msemaji wa wizara hiyo, Robert Palladino alisema juzi kwamba Rais Tshisekedi atatembelea Washington hadi Aprili 5 mwaka huu ambako atakuwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo na maofisa wengine wa juu wa utawala wa Rais Donald Trump.
Hata hivyo msemani huyo alisema kuwa bado haijajulikana mara moja kama atakutana na Rais Trump.
“Tunaungana na matakwa ya Rais Tshisekedi ya kutaka kujenga uhusiano thabiti kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,” Palladino aliwaambia waandishi wa habari.
Alisema suala la kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa nchi hii kulikoghubikwa na vita litakuwa ni moja ya mambo yatakayojadiliwa.