Rais Tshisekedi kufanya ziara Marekani

0
624

KINSHASA,CONGO DR

WIZARA Mambo ya Nje   imesema kwamba Rais Felix Tshisekedi atafanya ziara mjini Washington DC  mapema mwezi ujao  kujadili kuimarisha uchumi na usalama.

Msemaji  wa wizara hiyo, Robert Palladino alisema  juzi kwamba Rais Tshisekedi atatembelea Washington hadi Aprili   5 mwaka huu  ambako atakuwa na Waziri wa Mambo ya Nje  wa Marekani,  Mike Pompeo   na maofisa wengine wa juu wa utawala wa Rais Donald Trump.

Hata hivyo msemani huyo alisema kuwa bado  haijajulikana mara moja kama atakutana na Rais Trump.

“Tunaungana na matakwa ya Rais Tshisekedi ya kutaka kujenga uhusiano thabiti kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,” Palladino aliwaambia waandishi wa habari.

Alisema suala la kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa  nchi hii  kulikoghubikwa na vita litakuwa ni moja ya mambo yatakayojadiliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here