29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Assoumani apata ushindi wa kishindo Comoro

MORONI,Comoro

RAIS  Azali Assoumani ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili katika maeneo mbalimbali nchini humu.

Kwa mujibu wa matokeo  yaliyochapishwa juzi jioni  na Tume ya Uchaguzi  yamempa Rais Assoumani  ushindi wa kishindo wa asilimia 66.77 ya kura.

Kwa ushindi huo, Rais Assoumani amemwacha mbali mpinzani aliyeshika  nafasi ya pili, Mahamoudou Ahamada ambaye kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa ameambulia asilimia 14.62 ya kura zilizopigwa, na kwa maana hiyo haitahitajika duru ya pili.

Hata hivyo hata kabla ya matokeo hayo kutangazwa, tayari upinzani ulikuwa umekwisha kuyapinga  ukidai kuwa upigaji kura uliandamwa na kasoro nyingi ambazo ziliripotiwa na tume ya uchaguzi.

Upinzani huo ulizilinganisha kasoro hizo na mapinduzi dhidi ya serikali, na kutoa wito kwa umma kusimama kidete na kuipinga hali hiyo.

 Ahamada alikwenda mbali na kuitaka Jumuiya za Kimataifa kutoutambua ushindi wa Rais Assoumani

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi,  Rais  Assoumani amekiri hitilafu zilijitokeza.

”Ni kweli makosa yalifanyika, lakini tunafurahi kwa sababu hali ingeweza kuwa mbaya zaidi,” alisema Rais Assoumani na kuongeza kuwa wanajipongeza, na kumshukuru Mungu na Wakomoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles