24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia awataka wanaozusha kuhusu kifo cha Magufuli wajitafakari

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaonya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza uzushi juu ya kifo cha Hayati Dk. John Magufuli kujitafakari.

Rais Samia ametoa maele “Mheshimiwa Spika jambo la pili ambalo nilitaka kulizungumza hapa, na hapa nikemee vikali wale walioko kwenye mitandao.

“Ndugu zangu ndimi zetu zinasema na ndio kanuni ya maisha, tunakuja duniani lakini tutaondoka duniani na dini zetu zinasema kila nafasi iliyokuja duniani itapatwa na mauti, lakini kila mauti yanasababu zake.

“Nimekuwa nikiona kwenye mitandao na nadhani wanafanya hivyo wanajua kwamba hatutaweza kuwapata wanatumia mifumo mingine ambayo bado hatujawa na uwezo wa kuwatafuta lakini niwambie tutawatafuta.

“Nimekuwa nikiona kwenye mitandao taarifa za uchonganishi, Taarifa tuliyopewa na Madaktari wetu ya kifo cha mpendwa wetu ( Hayati Dk. John Magufuli) nikutokana na tatizo la udhaifu wa moyo ambalo ameishi nalo kwa takribani miaka 10.

“Kuna watu wamejitokeza katika mitandao huko flani na flani wamempa simu, flani na flani walikutwa wametege kitu hiki, sasa mimi niwambie kama wanataarifa za maana waje tuwasikilize.

“Vyombo vya upelelezi na Uchunguzi vipo waje tuwasikilize, short of that(kifupi chake) wasisimame kuleta uchonganifu ndani ya nchi.

“Taarifa wanazozitoa za kugonganisha koo na koo, kwa kabila na kabila, waache kuleta uchonganishi ndani ya nchi lakini kama wanajidhatiti kwamba wanafanya hivyo na hatutawapata basi warudi tu kwa Mungu wao, wakajiulize kama hili wanalolifanya linauhalali au linamaana gani?

“Warudi tu kwa Mungu kwa sababu ni viumbe pia, warudi kwa Mungu wakajiulize tunayoyafanya ndiyo? Wangeambiwa wao hivyo wangekubali, kwa hiyo mheshimiwa Spika nilikuwa nitumie jukwaa lako hili kukemea hayo,” amesema Rais Samia Suluhu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles