24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS ROUHANI ASHINDA KWA KISHINDO

TEHRAN, IRAN


RAIS Hassan Rouhani amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kuzoa asilimia 57 ya kura, ikiashiria kuungwa mkono kwa juhudi zake za kujenga upya uhusiano wa kigeni wa nchi hiyo.

Sheikh huyo mwenye umri wa miaka 68, ambaye alimshinda mpinzani wake mkuu mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi alitumia miongo mitatu katika kitovu cha utawala wa kimapinduzi wa Iran.

Lakini bado anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wale wenye misimamo mikali wakati akijaribu kujenga upya uhusiano na mataifa ya magharibi.

Rouhani ambaye daima amekuwa akivaa kilemba cheupe amerudia tena ushindi wake wa kishindo alioupata mwaka 2013 kwa kuwaunganisha pamoja wafuasi wa misimamo ya wastani na wanamageuzi kwa ahadi ya kukomesha kutengwa kwa Iran na kuboresha haki za kiraia nchini Iran.

Rouhani mwenye mke na watoto wanne ambaye ana shahada ya uzamivu ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Caledonia cha Glasgow, Scotland alijinadi kama mgombea wa mabadiliko na uhuru wa kijamii kwa kuwashambulia wapinzani wake kuwa watu wenye misimamo mikali, ambao enzi yao imekwisha.

Muhula wake wa kwanza umeshuhudia kufikiwa kwa makubaliano ya kihistoria na mataifa yenye nguvu duniani ambayo yamekomesha vikwazo vingi na mzozo wa miaka 13 kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Pia ameanzisha mtizamo wa kisomi zaidi katika kuushughulikia uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei uliokuwa ukiongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles