27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MALINZI WAMEANZA KUKUELEWA KIMYA KIMYA

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


MSINGI wa mafanikio ya timu za Taifa duniani kote ni kuwekeza katika soka la vijana ili kuhakikisha vijana hao wanafundishwa soka kwa kiwango cha kimataifa kuanzia wakiwa wadogo.

 Wakilelewa pamoja na kufundishwa mpira pamoja ukubwani wanaunda Timu ya Taifa imara yenye uwezo wa kushindana na timu yoyote duniani. Hakuna njia ya mkato.

Kwa kipindi kirefu Tanzania haijafanikiwa kucheza fainali kubwa za mpira Barani Afrika. Mara ya mwisho kupata mafanikio makubwa kwa Timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) ilikuwa ni mwaka 1980, ilipofuzu kucheza fainali za Mataifa ya  Afrika (AFCON) nchini Nigeria.

Mwanafalsafa na mtunzi wa vitabu, Malcolm X aliwahi kusema: “Usiwe na haraka ya kutoa lawama kwa mtu kwa sababu ya kushindwa kufanya unachofanya au kufikiri kama wewe, kuna muda ambao haujui kama ambavyo unavyojua leo.”

Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukilinyooshea kidole Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kutokana na mapungufu yanayojitokeza lengo ni kuwakumbusha wahusika kuwa kuna sehemu wanakosea hivyo wanahitaji kujitathmini na kuboresha mapungufu hayo.

Wapo ambao walikuwa hawalali wakikesha kulinyooshea kidole shirikisho hilo, hasa Rais wake, Jamal Malinzi, wakidai amechangia kushushsa  kiwango cha soka nchini.

Kama tujuavyo kwamba upo uchafu lukuki unaotokana na baadhi ya mapungufu yanayojitokeza katika uendeshaji wa shirikisho hilo chini ya Malinzi.

Dosari za waamuzi, upangaji matokeo, rushwa, uduni wa viwanja, upendeleo wa klabu za Simba na Yanga pamoja na  kushuka kiwango kimataifa ni baadhi tu ya vitu vinavyochangia Malinzi kuonekana hafai kabisa kuliongoza soka letu.

Lakini kwa hili la Timu ya Taifa ya vijana ya ‘Serengeti Boys’ kufanya vizuri na kuwa mbioni kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Dunia la vijana mwakani, linaweza kufuta yote mabaya na kutuunganisha tena baada ya kutofautiana kwa  kipindi kirefu.

Kwani maendeleo yanayoonekana sasa ya timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 dhahiri inatupa picha ya huko tuendako kutokana na uimara na ubora wao.

Juhudi hizi za Malinzi na safu yake ya uongozi zinaonekana kuanza kuwafuta machozi Watanzania baada ya muda mrefu kupita bila ya mafanikio yeyote ya michuano ya kimataifa.

Wapo baadhi ya Watanzania ambao wataendelea kukosoa kwa kile kinachofanyika, lakini bila shaka watakuwa wakianza kuelewa nini hasa kusudio la Malinzi kwenye maendeleo ya soka nchini.

Kwa hakika Malinzi alitupa shida ya kumuelewa hapo awali kutokana na mwelekeo wa soka kuwa mbaya zaidi, hasa matukio ya ajabu na aibu ambayo yalilitia kinyaa soka letu.

Si kwamba yamepungua au kuondoka, ila kwenye uso wa kusukuma ngozi kwa upande wa vijana tunaweza kuanza kukenua, huku tukiwa tunanyooshana taratibu wenyewe kwa wenyewe hadi kieleweke.

Msingi wa hapa tulipofika unatokana na kusemana na kurekebishana kwa kuwa lengo kuu ni kutaka kufika katika hatua ya kimataifa kama ambavyo wenzetu wamefika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles