31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS PUTIN KUKUTANA NA WANAHABARI WA KIMATAIFA

MOSCOW, Urusi


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin anatarajia kukutana na wanahabari mahiri wa kimataifa katika mkutano wake wa kila mwaka na vyombo vya habari Alhamisi wiki hii.

Mkutano huo utakaofanyika Alhamisi wiki hii utamkutanisha na wanahabari 1,640 kutoka mataifa mbalimbali kama vile Marekani, Ujerumani, Japan, Ufaransa, China, Poland, Estonia, Urusi na kwingineko.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hapa juzi na msemaji wa Ikulu, miongoni mwa wanahabari hao ni Ksenia Sobchak wa Kituo cha televisheni cha Dozhd, ambaye anajiandaa kupambana na Putin katika uchaguzi wa rais wa Urusi.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Sobchak kuhudhuria mkutano huo wa Rais Putin baada ya kufanya hivyo mwaka  2014  na 2015.

Mbali na mwandishi huyo mwingine aliyetajwa ni mtangazaji wa kituo cha Redio Ekho Moskvy, Tatiana Shadrina, ambaye Oktoba mwaka huu alishambuliwa na raia kutoka Israeli.

Rais Putin alilaani vikali tukio hilo na kusema kuwa hana cha kulizungumzia zaidi kutokana uhuru wa kujieleza uliopo nchini hapa.

Mkutano huo wa kila mwaka wa Rais Putin na wanahabari unazidi kupata umaarufu, ukiongezeka kwa mahudhurio kutoka waandishi 500 mwaka 2001, hadi idadi ya sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles