Kisumu, Kenya
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema nchi yake iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na Kenya pamoja na jamii ya kimataifa.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akiwa na mwenyeji wake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mji wa Kisumu, Rais Ndayishimiye alimshukuru rais Kenyatta kwa mchango wake katika mchakato wa kuleta amani nchini mwake.
Ndayishimiye ameelezea jinsi Burundi ilivyofanya mageuzi ili kuvutia wawekezaji wa kigeni ikiwemo kuwezesha mtu kufungua kampuni chini ya saa 24 .
Rais Ndayishimiye amewakaribisha wawekezaji kutoka Kenya akisema kuna fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za Kilimo, Utalii, Kawi, madini na Benki.
Pia Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Kenya, Raila Odinga alituma ujumbe kupitia moja ya mtandao wa kijamii ambapo alielezea kuwa Ndayishimiye atakuwa mgeni wa heshima katika sikukuu ya Madaraka, ambapo Wakenya husherehekea siku ya taifa lao lilipojitawala lenyewe kwaka 1963 baada ya kuwa chini ya utawala wa muingereza tangu mwaka 1920.