25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Rais MasterCard Afrika ashuhudia Droo ya 5 NMB MastaBata

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

RAIS mpya wa MasterCard International Kanda ya Afrika, Mark Elliott, leo Alhamisi Februari 3, ameshuhudia droo ya wiki ya tano ya Kampeni ya NMB MastaBata, ambako washindi 100 wamejishindia jumla ya Sh milioni 10, hivyo kufanya pesa zilizotolewa kwa washindi 525 kufikia sh milioni 75 Kati ya zaidi ya sh milioni 200 zinazoshindaniwa.

NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ ilianza mwishoni mwa Desemba 2021, ambako kila wiki washindi 100 hutafutwa kupitia droo zinazosimamia na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT). Washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi hujishindia Sh milioni 1 kila mmoja, huku wana fainali 30 wakitarajiwa kujinyakulia Sh milioni 3 kila mmoja hapo Machi mwishoni.

Kampeni hiyo ya wiki 10, inahamasisha matumizi ya kadi za MasterCard, Masterpass QR na Vituo vya Mauzo (PoS), ambako tayari washindi 525 Kati ya 1,080 wamejinyakulia Sh milioni 75 kati ya zaidi ya Shmilioni 200 zinazoshindaniwa.

MasterCard ni washirika wa kibiashara wa NMB, ambako mwaka jana 2021 Kampuni hiyo iliitunukia NMB Tuzo ya Benki Kinara Katika Kuhamasisha Matumizi ya Kadi, ambako Rais Mark Elliott, ameshuhudia moja ya droo za kampeni mbalimbali za kuhamasisha matumizi hayo yasiyohusisha pesa taslimu.

Rais Elliot ambaye ni mpya madarakani, ametembelea NMB kujionea huduma mbalimbali na shughuli za kiutendaji na kiuendeshaji kwa jumla, ambako amekiri kuvutiwa na Kampeni ya MastaBata na huduma za benki hiyo kwa ujumla.

Akizungumza kabla ya droo, Meneja wa Idara ya Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema tayari washindi 400 wa droo za kila wiki walishatwaa Sh milioni 40, huku washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi Januari wakijinyakulia Sh milioni 25, hivyo kupatikana kwa washindi 100 wa droo ya 5, kuigawa kampeni hiyo nusu kwa nusu kuelekea ‘Grande Finale’ mwishoni mwa Machi mwaka huu.

“Tayari washindi 400 wamenufaika na Sh 100,000 kila mmoja kwa droo za mwisho wa wiki, sambamba na washindi 25 wa Januari waliojinyakulia Shmilioni 1 kila mmoja. Tuko katikati ya kampeni yetu, kwani tumebakisha wiki 5, droo moja ya mwisho wa mwezi Februari, pamoja na fainali mwishoni mwa kampeni hii.

“Wito kwa Watanzania ni kuchangamkia fursa za kujishindia motisha hizi. Wenye akaunti waendelee kutumia kadi zao kufanya miamala, malipo na manunuzi, na wale wasio na akaunti, wajitokeze matawini kufungua na kuomba kadi, ili kukidhi kigezo kikuu cha ushiriki wa kampeni hizi na kunufaika na zawadi za pesa taslimu,” amesisitiza Mwamwitwa.

Droo hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa GBT, Joram Mtafya, ambaye aliwahakikishia wateja wa NMB kuwa, kampeni hiyo inaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zinazotambuliwa na bodi yake na kwamba uwepo wake hapo ni mfululizo wa utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakikisha washindi wanapatikana kihalali, huku akiwatoa hofu wateja wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles