24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI KUONGEZA NDEGE NNE ZAIDI

air-tanzania-q400

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amesema Serikali inatarajia kununua ndege nne kutoka kampuni mbili tofauti ambazo zinatarajia kuwasili nchini kati ya Mei na Juni 2017.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema   Rais   aliyasema hayo alipokuwa na  mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji Ndege ya Boeing ya Marekani, Jim Deboo.

Msigwa alisema Rais alitaja aina ya ndege mpya ambazo Serikali itazinunua kuwa ni Bombardier Dash 8 NextGen, ndege mbili Bombadier CS300 zenye uweza wa kubeba abiria 137 na 150 na Boeing 787 Dash 8 Dream Liner ya abiria 262 ambazo zote zinatarajiwa kuwasili kati ya Mei na Juni 2017.

Alisema malipo ya  awali yamekwisha kufanyika.

“Sisi hapa tunazungumzia kuwa na watalii hawajafika hata milioni mbili kwa mwaka, lakini nchi kama Moroco inapata watalii zaidi ya milioni 12, hali hii ni kwa sababu hatuna mashirika ya ndege.

“Watalii wa kuja kwa kuungaunga na wanafikia nchi nyingine halafu watapataje moyo wa kuja huku licha ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano zenye maeneo mazuri ya utalii.

“Kwa hiyo niwaombe Watanzania wapende mali zao kwa sababu wakati mwingine nikiangalia mitandaoni na magazeti ni ajabu huwezi kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta wanasifu ndege za watu na wanabeza za kwao.

“Tumeleta Bombadier zimepunguza gharama za safari. Mfano kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza ni kati ya Sh 160,000 na Sh 200,000 wakati nauli ilishafika Sh 800,000   lakini hawaishi kuzungumza maneno ya ovyo kwa kutumiwa…tumeshaamua na tutafanya hivyo,” alisema Rais Dk. Magufuli.

Wakati huo huo, taarifa hiyo ilisema Rais Dk. Magufuli aliagana na aliyekuwa Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini (AfDB), Dk. Tonia Kandiero ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Kusini mwa Afrika.

Pia baada ya mazungumzo na Dk Tonia Rais Dk Magufuli aliagana na Balozi wa Ciba nchini, Jorge Luis Lopez Tormo aliyemaliza muda wake wa miaka mnne.

Mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles