26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli kufanya ziara ya siku tatu Dar

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ambapo katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amesema ziara hiyo itaanza Jumatano ya Februari 24, ambapo Rais Dk. Magufuli atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na Mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwaajili ya uzinduzi wa Kituo Cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

Aidha, Kunenge amesema Siku ya Alhamis ya Februari 25 Rais Dk. Magufuli ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 Asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambapo Kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.

RC Kunenge amesema Siku ya Ijumaa ya Februari 26 Mhe. Rais atafanya shughuli ya uzinduzi wa Majengo ya chuo cha Polisi na Kiwanda cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika Saa 03:30 asubuhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles