28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli awapunguzia adhabu wafungwa

Na Richard Deogratius, Dar es Saaam

Rais Dk. John Magufuli, amewapunguzia kifungo wafungwa 256 wa kesi mbalimbali, waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Desemba 9, mara baada ya hafla ya kuwaapisha Mawaziri 21 na Manaibu 23 wanaounda Baraza jipya la Mawaziri, ililofanyika Ikulu jijini Dodoma.

“Najua katika kipindi cha miaka mitano mpaka leo nilitakiwa niwe nimenyonga watu 256, waliohukumiwa kunyongwa, sijanyonga hata mmoja na wale 256 kwa mamlaka niliyopewa nawapunguzia kifungo chao, cha kunyongwa sasa wafungwe maisha.

“Kwa sababu hao wapo walio hukumiwa kunyongwa kwa sababu waliuwa, labda mwingine aliuwa mmoja au mwingine aliuwa wawili au mwingine aliuwa watatu, mimi sheria inaniambia niuwe 256 nani mwenye dhambi zaidi huyu aliyeuwa mmoja, wawili au mimi nitakayeuwa 256.

Pia ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani kushughulikia swala hilo kwa mujibu wa taratibu na Sheria zote kwa wale wote waliohukumiwa kunyongwa 256 wafungwe maisha na washiliki katika kufanya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles