23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai: Msilewe madaraka kwa kuitwa Waziri –

Na Faraja Masinde

Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka Mawaziri na manaibu walioapishwa leo Desemba 9, kutokulewa sifa ya madaraka na badala yake wakajitahidi kuacha alama.

“Ndugu zangu mmepewa madaraka, mkajitahidi sana siku yoyote mkitoka kwenye madaraka haya, muache alama, muache kumbukumbu za kudumu katika mioyo ya Watanzania kwamba mliwahi kupata nafasi hizo.

“Wengine mlikuwa na madaraka hayohayo, kabla ya kuanza upya kageuke nyuma utathimini, uangalie ulipopata nafasi hii huko nyuma ulifanya nini na unapoenda huko mbele una nini cha kufanya.

“Msiende mkalewa na madaraka ya kuitwa waziri, mkumbuke nafasi mliyopewa ni ya utumishi wa Watanzania, hili la Utumishi likatangulie mbele zaidi, tusaidiane ili kwa pamoja inapofika 2025 Mwenyezi Mungu akijalia tukawa pamoja sote basi tukaione Tanzania iliyona mabadiliko makubwa zaidi. Ni muhumu sana mkahudhuria vikao vya bunge, niwajibu wenu tena wa kikatiba kuhudhuria vikao vya bunge,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Desemba 9, kwenye hafla ya uapishwaji Mawaziri 21 na Manaibu 23 iliyofanyika Ikulu jijini Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles