25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI AWANYOSHEA KIDOLE, KAIRUKI, TIZEBA

Na LEONARD MANG’OHA- DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli, amewanyoshea kidole Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Charles Tizeba na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, kuhusu mwenendo wao wa utendaji kazi.

Mawaziri hao, walinyoshewa kidole Ikulu, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko.

Kuhusu Tizeba, Rais Magufuli alisema haiwezekani hadi sasa baadhi ya mikoa, ikiwamo inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula, kushindwa kupata mbolea, huku yeye yupo bila kuchukua hatua.

“Ninapozungumza hapa ndugu zangu, ipo mikoa haijapelekewa mbolea, ikiwamo mikoa ya Rukwa sijui na mkoa gani.

“Wakati tunaizungumzia kama ‘the big four’ kwa ‘production’ ya chakula, mbolea bado haijapelekwa, lakini Waziri wa Kilimo yupo.

“Nimempa maagizo Waziri Mkuu mbolea isipofika huko ndani ya wiki hii, huyo anayehusika na kupeleka mbolea aachie kazi, labda tukianza kukimbizana tutajifunza, nilishasema wale wote ninaowateua mimi wasifikiri mchezo, wanakuja kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli.

Alisema mtu yeyote anayemteua akiona hawezi kufanya kazi, asikubali kuteuliwa kwa sababu uteuzi wake unalenga kutatua matatizo ya wananchi.

 

WAZIRI KAIRUKI

Akionekana kuzungumza kwa hisia, Rais Magufuli alionekana wazi kutoridhishwa pia na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Kairuki na kutaka afikishiwe salamu zake kwa sababu yuko likizo.

Alisema tangu Sheria ya Madini mwaka 2017, Wizara ya Madini haijamshawishi na aliwaagiza watendaji wa wizara hiyo kumfikishia waziri salamu kuwa bado hajamshawishi.

“Baada ya kupitisha hiyo sheria, ilipofika tu mezani siku hiyo hiyo niliisaini, nikatoa maagizo watendaji wangu washughulikie ‘regulation’, sasa kuanzia mwezi wa saba baada ya kupitisha mwaka 2017, mpaka leo hazijasainiwa.

“Waziri yupo, naibu waziri yupo, kamishna ambaye ndiye mshauri mkuu wa madini yupo, wakurugenzi wapo, unaweza ukajiuliza kuna matatizo makubwa katika hii Serikali kwa sababu kama zile ‘regulation’ hazijasainiwa unategemea nini?

“Tusipokuwa na ‘regulations’, mtu yeyote aki-deport atampeleka kwenye mahakama ipi, sisi Watanzania, baadhi ya watendaji serikalini ‘they are not serious’, ninasema hivi kwa uchungu mkubwa.

“Sifahamu Wizara ya Madini ina ugonjwa gani, mtu unamteua pale, sioni hiyo ‘movement’ ninayoitaka ‘and this is facts’, sioni,” alisema.

Aliwataka viongozi wa Wizara ya Madini kumtanguliza Mungu kupambana na mapepo kama madini yanayowafanya viongozi wanaopewa wizara hiyo kubadilika.

 

AMTUMBUA KAMISHNA

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alimtumbua Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, na kumteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Shukuruni Manya kushika nafasi hiyo.

“Nilikuwa naambiwa kamishna ni tatizo, inawezekana yuko hapa amekuja kumpokea naibu waziri, nimeamua kuteua mtu fulani hivi, sijui nitalikumbuka jina lake, lakini la kwanza linaanza na Profesa Shukuruni Elisha Manya nafikiri.

“Ni mwalimu wa chuo kikuu, ni geologist, nililetewa mapendekezo ya watu wa palepale nikaona ngoja nisichukue kabisa hapa, ‘we should start with a new page’, mtu ambaye hajawa ‘contaminated’, kwani huyo ndiye atakuwa Kamishna Mkuu na atakaimu kama Mtendaji Mkuu wa Kamishna wa Madini ili kusudi mambo yaanze ‘ku-move’ mapema,” alisema.

Rais Magufuli alisema kuendelea kuwapo kwa kasoro mbalimbali kunaonyesha wateule wake bado hawajamwelewa anataka nini na wananchi wanataka nini.

“Sekta ya madini ipo, tumeingia kwenye mazungumzo makubwa, nashukuru tume iliyofanya hiyo kazi, mazungumzo yameenda vizuri, itaanzishwa kampuni ya Serikali, sasa jambo baya ‘regulations’ hatujatengeneza, alafu kamishna anawapendelea wale badala ya kuipendelea Serikali, tujifunze sisi viongozi kuwa watu wa mfano kwa wananchi wetu, kazi hii ndugu zangu ni mateso na msalaba mkubwa,” alisema.

 

KANUNI

Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi, kusimamia na kusaini kanuni hizo, ikiwa utaratibu unamzuia Naibu Waziri wa Madini kufanya hivyo.

“Sasa mmekuwa manaibu waziri wawili na waziri mmoja, nitashangaa sana hii wizara kama hizi ‘regulations’ hazitasainiwa tena, Waziri wa Sheria yuko hapa, leo ni Jumatatu, nataka kabla ya Ijumaa wiki hii hizi ‘regulation’ ziwe zimesainiwa,” aliagiza.

 

UTEUZI WA BITEKO

Kuhusu uteuzi wa Biteko, alisema amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kuchunguza sakata la madini ya Tanzanite na namna ambavyo amekuwa akiiongoza Kamati ya Bunge ya Madini……

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles