28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Kenyatta awaagiza maafisa, mawaziri kupata chanjo ya corona

Nairobi, Kenya

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewaagiza mawaziri wote na maafisa wakuu serikalini wawe kielelezo kwa kupokea chanjo dhidi ya corona.

Maafisa kadhaa wakuu katika serikali akiwemo Mkuu wa Wafanyakazi katika Ikulu, Nzioka Waita ni miongoni mwa waliochanjwa.

Kupitia Ujumbe wa Twitter uliokuwa na picha akipokea chanjo hiyo Waita amethibitisha maelekezo hayo ya rais kuhusu kuchanjwa kwa maafisa wakuu.

Hatua hiyo ni kinyume na msimamo wa hapo awali wa serikali kwamba wanasiasa hawataruka foleni kwa kuchanjwa kwanza kabla ya makundi ya watu wengine waliopangwa kuchanjwa mwazoni.

Waziri wa Afya nchini humo, Mutahi Kagwe, amesema Wakenya milioni 1.25 watapokea dozi ya shehena ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca na wanasiasa sio miongoni mwa watakaopewa chanjo hiyo .

Kumekuwa na hofu miongoni mwa Wakenya kuhusu usalama wa chanjo ya Corona na serikali imechukua hatua za uhamasishaji ili kuwarai watu kwenda kuchanjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles