23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

CDF Mabeyo: Nchi iko salama, tutakulinda

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo ameahidi utiifu kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu.

Mabeyo amemhakikishia kuwa ulinzi wa nchi na mipaka yake ni salama na vitaendelea kumlinda, kumtii kama Amiri Jeshi Mkuu na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

‘’Tunakuahidi utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kama ilivyo ada ya mila na desturi ya majeshi yetu katika awamu zote zilizopita kwa manufaa ya ulinzi, usalama na ujenzi wa taifa letu,” amesema Jenerali Mabeyo.

Jenerali Mabeyo amesema hayo leo Ijumaa Machi 26, mjini Chato wakati akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Amirijeshi Mkuu.

Kuhusu namna alivyomfahamu na kufanya naye kazi hayati Magufuli Jenerali Mabeyo alisema; ‘’Aliviamini na kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama alihakikisha kuwa anaviwezesha kwa mahitaji ya kiutendaji na utawala ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi mkubwa.

“Alisema hatuwezi kuwa na vyombo vya ulinzi imara bila kuwa na uchumi madhubuti, hatuwezi kutegemea misaada ya kuimarisha vyombo vyetu lazima tuimarishe uchumi wetu ili tuweze kuimarisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama,” amesema Mabeyo.

Mabeyo amesema walishiriki katika kulinda mgodi wa Tanzanite, na kabla ya kulinda, kujenga ukuta kuzunguka mgodi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles