HATIMAYE jina la Thomas Tuchel liko mikononi mwa Rais wa Barcelona, Joan Laporta, ambaye anasaka kocha wa kuchukua nafasi ya Ronald Koeman.
Koeman raia wa Uholanzi atafukuzwa hivi karibuni na Tuchel wa Chelsea anaungana na Marcelo Gallardo, Xavi, na Roberto Martinez katika orodha ya makocha wanaotajwa Camp Nou.
Hata hivyo, bado Tuchel ana mkataba na vigogo wa Stamford Bridge na utamalizika mwaka 2024.
Aidha, taarifa za Barca kuitaka huduma ya Tuchel zinakuja huku zikiwapo pia zile zinazodai mabosi wa klabu hiyo wanammezea mate Mjerumani mwingine anayefanya kazi England akiinoa Liverpool, Jurgen Klopp.