24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

PSPTB yatangaza matokeo ya mitihani ya 20,21 na 22

*Yaonya wanaofanya kazi bila kusajiliwa

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) imeidhinisha matokeo ya watahiniwa 2,108 waliofanya mitihani ya 20, 21 na 22 katika ngazi mbalimbali za masomo ya fani hiyo.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo Jumatano Januari 19, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kwa upande wa mitihani ya 20 ambayo ilifanyika Agosti mwaka 2020 watainiwa waliofanya mtihani hiyo walikuwa ni 1,060 ambapo waliofaulu  ni 479 ambao watakuwa na mitihani ya marudio ni 519  huku waliofeli kabisa na wanatakiwa kurudia mitihani yote ni 62.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa anatangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya 20,21 na 22 yaliyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB makao makuu ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mbanyi amesema kwenye mitihani ya 21 iliyofanyika Novemba mwaka 2020 watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa ni 571 ambapo watahiniwa waliofaulu ni 216 ambao watakuwa na mitihani ya marudio  ni 321  na waliofeli kabisa ambao wanatakiwa kurudia mitihani yote ni 34.

Amesema mitihani ya 22 iliyofanyika mwezi Juni mwaka 2021 watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa ni 477 ambapo watahiniwa waliofaulu 165 ambao watakuwa na mitihani ya marudio  ni 262  na waliofeli kabisa ambao wanatakiwa kurudia mitihani yote ni watahiniwa 50.

“Jumla ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo walikuwa ni 2,108 ambapo watahiniwa 860 wamefaulu mitihani ya bodi, watahiniwa 1,102 wamefeli somo moja au zaidi ambapo watakiwa kufanya marudio ya mitihani hiyo na waliofeli jumla yake ni 146 na hao wanatakiwa kurudia mitihani yote ya bodi,” amesema Mbanyi.

Aidha, amesisitiza kuwa taarifa za matokeo haya zinapatikana kwenye tovuti ya Bodi hiyo ambayo ni www.psptb.go.tz ambapo mtahiniwa anaweza kuona matokeo yake kupitia akaunti yake.Pia dirisha la usajili kwa ajili ya mitihani ya Mei, 2022 linafunguliwa kuanzia terehe 24/01/2021.

Katika hatua nyingine Bodi hiyo imewakumbusha wale wote wanaofanya kazi ya taaluma hiyo bila kusajiliwa na bodi kufanya hivyo mapema kwani kinyume chake nikukiuka sheria.

Katika hatua nyingine bodi hiyo imesema kuwa waliosajiliwa kwa mwaka huu ni 1,055 ikilinganishwa na 1,166 waliosajiliwa mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles