24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wahitimu watakiwa kuchangia shule waliyosoma

Na Malima Lubasha, Serengeti

WANAFUNZI waliosoma shule ya msingi Kichongo Wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kujitokeza kuendelea kuchangia ukarabati ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo  ili kuimarisha mazingira rafiki ya kujifunzia.

Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Butiama, Chacha Megewa wakati akizungumza na Walimu, Wazazi, Wananchi na wadau katika harambee ya kuchangia ukarabati wa majengo ya shule hiyo iliyofanyika jana katika viwanja vya shule.

Alisema ni wajibu wa wahitimu ambao tyari amshapata nafasi kwenye taasisi za umma na binafsi ni vyema wakazikumbuka shule walizosoma ikiwemo wale waliopita shule ya Msingi Kasongo.

Megewa aliwataka wazazi wa eneo hilo kuwaunga mkono wanafunzi waliosoma shule hiyo baadhi wakiajiriwa Serekalini wengine wakiwa wafanyabiashara kuanzisha group la kuchangia ukarabati wa majengo.

Megewa aliwapongeza wanafunzi waliosoma shule hiyo kuanzia mwaka 1981 hadi 1989 kubuni wazo hilo la kuunda kikundi “KICHONGO YETU” kuchangia ukarabati wa majengo huku shule ikitimiza umri wa miaka 58 ambapo wanafunzi zaidi ya 745 waliosoma hapo walifaulu kwenda sekondali hadi mwaka 2021.

Katika harambe hiyo fedha taslimu zilizopatikana ni zaidi ya Sh milioni 3 wengine waliahidi kutoa saruji, rangi na mbuzi ambapo uongozi wa shule uliagizwa kuhakikisha fedha zilizopatikana zinatumika kama zilivyopangwa.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kichongo Mang’era Mwita alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1964 chini ya mpango wa Twiboki hadi 1973 ilipokabidhiwa Jumuiya ya Wazazi TAPA ambapo mwaka 1975 ilikabidhiwa Serikalini na kupata usajili wa kudumu.

Mwita alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 835 na walimu 8 inakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuzitaja kuwa ni upungufu wa madawati 110 nyumba za walimu 12 na walimu 13 wanahitajika pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo 3 kwa walimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles