27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Programu ya usafiri ya Linkee yazinduliwa Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Programu mpya ya usafiri ya Linkee imezinduliwa jijini Dar es Salaam hatua itakayowezesha wakazi wa Jiji hilo kuondokana na adha ya usafiri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo Jumatatu Novemba 29, 2021 jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa hiyo itakuwa ujio wa programu hiyo mbali na kiurahisisha usafiri pia utasaidia kutengeneza kipato kwa vijana wa kitanzania wanaojishughulisha na udereva.

“Linkee pia inatoa uwezekano wa kufikia bei zinazolingana kwa sababu kwa miezi sita ya kwanza kutoka uzinduzi, dereva hatakatwa fedha yoyote na kwamba mfumo huo utakuwa wa wazi.

“Lakini pia kupitia Linkee App, watumiaji pia wataweza kuomba aina mbalimbali za usafiri kama vile magari, bodaboda, na bajaji jijini Dar es Salaam. Pia madereva watakuwa na uhuru wa kuchagua safari, ama kwa bei, wasifu wa kihistoria wa abiria kwenye jukwaa, unakoenda, au wakati wa siku; kufanya Linkee kuwa moja wapo ya programu zinazonyumbulika zaidi sokoni kwa wajasiriamali,” imeeleza taarifa hiyo.

Programu tumishi hiyo(APP) imetengenezwa maalumu kwa ajili ya Tanzania ili kusaidia jamii kuboresha maisha kupitia teknolojia.

Aidha, kampuni hiyo inawaalika madereva na abiria jijini Dar es Salaam kuchangamkia fursa hiyo huku ikiahidi ofa mbalimbali kwa wateja wake wa mwanzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles