32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA TIBAIJUKA ATAJA CHANZO MAFURIKO DAR

KAMILI MMBANDO-DAR ES SALAAM


MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) ameeleza kuwa tatizo la mafuriko   Dar es Salaam ni wanasiasa kutothamini kazi za wataalamu wa mipango miji.

Profesa Tibaijuka ameyaeleza hayo wakati huu ambao jiji la Dar es Salaam limekumbwa na adha kubwa ya mafuriko kutokana na mvua inayoendelea kunyesha   na kusababisha vifo kadhaa,  watu wengine kukosa mahali pa kuishi na barabra kufungwa hasa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani.

Katika taarifa yake aliyoituma kwenye mitandao ya  jamii juzi, Mbunge huyo alisema   tatizo la mafuriko halitokani na wataalamu bali ni wanasiasa  kukosa utamaduni wa kuheshimu wataalamu   na wananchi kutaka njia rahisi.

Alisema tatizo hilo la mafuriko halitaweza kuisha kwa sasa mpaka  utakapotekelezwa  mpango maalum wa jiji hilo (master plan) wa mwaka 1979 wakati wa uongozi wa Mwalimu  Nyerere ambao ulionyesha jinsi ya kumaliza tatizo la mafuriko   Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ya Profesa Tibaijuka ilieleza kuwa kama hakutakuwapo na nidhamu ya kuheshimu wataalamu wa mipango miji, mafuriko yataendelea kuwa tatizo sugu na  la muda mrefu katika jiji hilo.

“Tatizo si mvua kubwa, tatizo ni kuziba  njia za asili zinazotiririsha maji kwenda baharini.

“Nilipokuwa Wizara ya Ardhi, nilijitahidi kuokoa Bonde la Mto Msimbazi kwa mujibu wa  master plan1979 ambayo ilikuwa ni ya Nyerere, sikuweza kufanikiwa… bonde likaendelea kujengwa na maji hayana njia nyingine ya kufika baharini.

“Fikiria Bonde la Msimbazi (mto) ndiyo njia pekee ya maji yote yanayotoka Pugu, Hills, Ukonga, Airport, Tazara, Tabata, Kigogo, Magomeni, Ilala kufika Jangwani katika mizunguko hadi daraja la Salendar.

“Vile vile maji kutoka Ubungo, Manzese, Tandale, Magomeni Kagera, Kinondoni Hananasifu, Muhimbili hadi Jangwani na njia ni hiyo tu moja huku kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukiwa na Mto Mbezi, Mto Mlalakuwa na Mto Mdumbwi na eneo la Kawe likiwa limejengwa kwenye njia za maji,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles