31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MAJAJI HEWA 250 WAFUTWA KAZI DRC

KINSHASA, DRC


SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imewafukuza kazi zaidi ya mahakimu 250 waliokuwa wameajiriwa kwa kutumia vyeti feki na wengine waliotuhumiwa kupokea hongo.

Tume maalumu iliundwa kufuatilia maofisa katika idara mbalimbali, ambao hawana sifa ya kufanya kazi ya uhakimu au nyinginezo za kitaalamu serikalini.

Rais Joseph Kabila aliwafukuza kazi mahakimu hao kwa kile alichosema kosa kutumia vyeti bandia na wengine kwa tuhuma za kupokea rushwa wakati wa kesi mbalimbali.

Hatua hii inafuata malalamiko mengi ya wananchi pia kutokana na utendaji wao mbovu.

Mara kwa mara mashirika ya kiraia yamekuwa yakilalamika utendaji wa mahakama na hatua ya kuwatimua inaonekana kuwa moja ya majibu hayo, anasema Dufina Tabu mratibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu nchini Congo (Savoco).

‘Tulikuwa tukimwandikia Rais barua na inaonekana zimefika. Kwa hivyo inakuwa ni mfano mzuri.

‘Maskini kupata haki yake kisheria ni vigumu. Kila kitu ni fedha. Watu wanateswa kupata haki na tutaendelea kumwunga mkono Rais. Kwa yoyote atakayefanya makosa tutamwandikia, tumtaje na aadhibiwe kabisa ili tuweze kuisaidia nchi yetu ipone’, alisema.

Hata hivyo, Waziri wa Sheria Alexi Tambwe Mwamba amesema tume maalum iliyoundwa kuendesha uchunguzi zaidi ya mahakimu ndiyo iliyogundua uwapo wa mahakimu feki.

Mara kwa mara rais Kabila ametangaza kuchukua hatua kukabiliana na rushwa nchini hapa, lakini wakosoaji wamekuwa wakiona hakuna ishara wala azma ya kisiasa na  uthibitisho wa hatua kupigwa katika kukabiliana na hilo, mbali ya kuundwa sheria kali, ambazo mara nyingi hazifuatwi.

Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu, Transparency International linasema ajenda ya kupambana na rushwa mara nyingi huingiliwa kati kwa maslahi ya kisiasa.

Rasilmali ni finyu kwa mahakama za nchi hiyo ambayo imeshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda sasa.

Na hiyo inamaanisha kuwepo kwa maafisa wasiotosha kukabiliana na mzigo wa mahitaji na pengine ndio kukatoa mwanya wa kuajiriwa majaji hao 250 hewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles