32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA NDALICHAKO: ADHABU SHULENI ZISITOLEWE KISIASA

profesa-joyce-ndalichakoNA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM

SERIKALI imeonya adhabu na maagizo ya shule visitolewe kisiasa bali kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Kamishna wa Elimu.

Vilevile, imewataka walimu kuwapa adhabu wanafunzi kulingana na mwongozo uliotolewa na serikali katika waraka wa adhabu wa mwaka 2002.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo   alipofungua   mjadala wa wanafunzi kuelekea  maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu, uliofanyika Makumbusho ya Taifa,  Dar es Salaam jana.

Alisema mwongozo huo unaeleza waziwazi aina ya adhabu anayostahili kupewa mwanafunzi husika kulingana na kosa alilotenda.

“Kwa mujibu wa mwongozo huo adhabu anayoweza kupewa mwanafunzi ni hadi viboko vinne, kulingana na kosa alilotenda maana wanafunzi wengine hutenda hadi makosa ya jinai kama vile wizi, uvutaji bangi na mengineyo.

“Mwongozo huo unaeleza kuwa anayepaswa kutoa adhabu hiyo ni mwalimu mkuu ingawa anaweza pia kuteua mwalimu mwingine atakayetoa adhabu kwa mwanafunzi husika.

“Walimu pia ni vema wakaweka na kutunza kumbukumbu ya adhabu aliyopewa mwanafunzi  iwe rahisi kufuatilia mwenendo wake, na hii itasaidia kupata viongozi bora wa baadaye,” alisema.

Waziri   alisema jamii kwa ujumla inapaswa kusaidia katika kuwalea watoto kwenye maadili yanayotakiwa kwa sababu  serikali peke yake haiwezi.

“Leo hii kuna viashiria vingi vya mmomonyoko wa maadili.

“Serikali ya awamu ya tano  inalipa kipaumbele suala la maadili lakini peke yake haiwezi.

“Kama jamii haitazingatia kujenga na kuwalea watoto katika maadili mema hata fedha zinazowekezwa kwenye elimu zitakuwa zimepotea bure,” alisema.

Aliwasihi wazazi kushirikiana kwa karibu na walimu  watoto wanapokuwa wakipewa adhabu na kuacha tabia ya kurudi upande wa watoto wao na kuwatetea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles