27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mkumbo: Rais siyo ofisa miradi

mkumboMSHAURI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo,  Profesa Kitila Mkumbo amesema   wananchi hawachagui rais ili awe ofisa miradi, meneja  au kufanya kazi za uhandisi kwa sababu wataalamu wa fani hizo wapo isipokuwa anayechaguliwa ni kiongozi mkuu wa nchi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara  katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam jana, Profesa Kitila alisema kazi za rais ni nne ambazo ni fikra kwa kuwa ndiye anayestahili kutoa dira ya nchi hivyo anatakiwa kuwa mwenye uwezo wa kufikiri sawasawa.

“Kila mnayemsikiliza lazima mumpime kwa uwezo wake na si kwa kumsikia, akisema kwamba ataleta maji au kujenga mitaro  kiongozi huyo mkataeni na mwambieni.  Sikuhitaji kwa kuwa wataalamu hao wapo na kama ukimuuliza atafanya akakujibu anasubiri ilani ya chama mkataeni kwa kuwa hana fikra za kuongoza nchi,” alisema.

Alitaja kazi nyingine ya rais   kuwa ni mlinzi Mkuu wa Tunu za Taifa za msingi kwa kuwa mlinzi wa umoja wa taifa na anatakiwa ajiepushe na tabia za udini na ukanda kwa kuwa ndiye mlinzi wa usawa; kulinda haki za walio wengi ambao ni masikini na asikubali kuwa mateka wa matajiri.

Tunu nyingine anayotakiwa kuilinda ni muungano ambao umelindwa kwa miaka 50, hivyo anatakiwa awe anaujua na asiwe na fikra za kuuchezea awe na uadilifu na mapambano dhidi ya ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles