25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Lipumba kuteta na Rais Kikwete

Pg 2Na Fredy Azzah, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya polisi kuwapiga wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema ataonana na Rais Jakaya Kikwete azungumze naye kuhusu jinsi Jeshi la Polisi linavyotumia nguvu dhidi ya raia na kufuta mashtaka dhidi ya wanachama wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema anashangazwa na hatu ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu na hata kuwapiga wanachama wa CUF bila hatia.
“Hali hii inatisha nitaenda kuzungumza na yule jamaa yangu (Rais Kikwete)… naongea na watu wanaomjua vizuri ili nipate nafasi ya kwenda kuongea naye, sintomwandikia barua kwa sababu huwa hana muda wa kusoma, nitaenda kuongea naye tushauriane vizuri.
“Nitamwambia hali hii ikiendelea hivi tuendako ni kubaya, wajue kwamba wananchi ni wengi kuliko hao polisi,” alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba alisema polisi waliamua kuwabambikiza kesi jambo ambalo linaendelea kupunguza imani kati ya chombo hicho na wananchi.
“Nitamwambia afute hizi kesi za kubambikiziwa, wananchi waliona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, huku polisi wanakuja kubambikiza kesi na serikali inatoa tamko bungeni wakidanganya umma waziwazi,” alisema.
Alisema licha ya kuwakamata na kuwapiga watu, polisi pia walitumia fursa hiyo kuiba vitu mbalimbali ikiwamo kamera.
“Safari hii mimi nimesalimika, sikuibiwa lakini kuna mwenzetu aliibia video camera, siyo tu waliiba ni kwamba wanapora hasa. Mimi Januari 25 mwaka 2001 waliponikamata waliniibia saa ya mkononi na mpaka leo nawadai,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles