26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mkuu apangua majaji

jaji_chandeNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande, amewahamisha majaji 27 wa Mahakama Kuu Tanzania akiwamo Jaji John Utamwa aliyehamishiwa Mahakama Kuu Tabora na Jaji Dk. Fauz Twaib aliyehamishiwa Mahakama Kuu Mtwara.

Uhamisho huo ulifanyika mwishoni mwa wiki ambako majaji wengine walibadilishwa vituo vya kazi na wengine kuteuliwa kuwa wafawidhi wa kanda.

Majaji waliohamishwa ni Jaji Agathon Nchimbi aliyekuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara kwenda Mahakama Kuu Ardhi, Jaji Sophia Wambura aliyekuwa Mahakama Kuu Kazi amehamishiwa Mahakama Kuu Ardhi Dar es Salaam.

Jaji Rehema Mkuye kutoka Mahakama Kuu Dodoma kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Jaji Kassim Nyangarika aliyekuwa Mahakama Kuu Biashara amehamishiwa Mahakama Kuu Sumbawanga.

Wengine waliohamishwa ni Jaji Hamisa Kalombola kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenda Mahakama Kuu Dodoma, Jaji Utamwa aliyekuwa Mahakama Kuu Dar es Salaam kahamia Mahakama Kuu Tabora, Jaji Richard Kibela alikuwa Mahakama Kuu Mtwara kahamia Mahakama Kuu Dar es Salaam, Jaji Haruna Songoro kutoka Mahakama Kuu Tabora kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.

Mbali na hao pia Jaji Dk. Twaib alikuwa Mahakama Kuu Dar es Salaam kahamishiwa Mahakama Kuu Mtwara, Jaji Salvatory Bongole aliyekuwa Mahakama Kuu Dar es Salaam kahamishiwa Mahakama Kuu Dar es Salaam Kituo cha Usuluhishi.

Jaji Jacob Mwambegele aliyekuwa Mahakama Kuu Sumbawanga amepelekwa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Jaji Latifa Mansoor alikuwa Mahakama Kuu Ardhi Dar es Salaam kahamishiwa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Jaji Lilian Mashaka aliyekuwa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi amehamishiwa Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.

Jaji Awadhi Mohammed kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenda Mahakama Kuu Dodoma na Jaji Dk. Modest Opiyo alikuwa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kahamishiwa Mahakama Kuu Arusha.

Majaji waliobadilishwa vituo vya kazi ni Jaji Amour Khamis alikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kapelekwa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Jaji Regina Rweyemamu alikuwa Divisheni ya Kazi kapelekwa Masjala kuu ya Mahakama Kuu, Jaji Richard Mziray alikuwa Divisheni ya Ardhi kapelekwa Masjala Kuu ya Mahakama Kuu na Jaji Sakieti Kihio alikuwa Kanda ya Dar es Salaam kapelekwa Masjala ya Mahakama Kuu.

Waliohamishwa kutoka kanda walizokuwapo ni Jaji Robert Makaramba alikuwa Divisheni ya Biashara Kanda ya Dar es Salaam kahamia Kanda ya Mwanza, Jaji Gad Mjemmas alikuwa Kanda ya Bokoba kahamishiwa Divisheni ya Biashara Kanda ya Dar es Salaam.

Wengine ni Jaji Aisheli Summari alikuwa kanda ya Mwanza kahamishiwa Kanda ya Moshi, Jaji Aisha Nyerere alikuwa Kanda ya Moshi kahamishiwa Divisheni ya Kazi na Jaji Stella Mugasha alikuwa Kanda ya Arusha kahamishiwa Kanda ya Dar es Salaam.

Majaji walioteuliwa kuwa wafawidhi ni Jaji Augustine Mwarija alikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kateuliwa kuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Biashara Kanda ya Dar es Salaam.

Wengine ni Jaji Sivangwila Mwangesi alikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kateuliwa kuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu na Jaji Amiri Mruma alikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kateuliwa kuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Tabora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles