26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Profesa Kitila aendesha uhakiki mita za maji

Na TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo ameungana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (Dawasa) kuhakiki na kusoma mita ili kuondoa udanganyifu katika Ankara za wateja.

Akizungumza katika uhakiki huo Profesa Mkumbo amesema lengo la kazi hiyo ni kuifanya DAWASA kuwa na taarifa sahihi za wateja.

“Zoezi hili litamsaidia mteja kujua kiasi cha maji ananitumia na kupunguza upotevu wa maji kwa mamlaka,” amesema.

Taarifa iliyotolewa na Meneja Mawasiliano kwa Umma Dawasa, Neli Msuya imesema kuwa wafanyakazi wa Dawasa watapiga Simu kwa wateja kupata taarifa zao.

Neli amewataka wananchi kuilinda miundombinu ya maji na kuhakikisha wanalipa Ankara zao kwa wakati ili huduma iwe endelevu.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles