24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Ndalichako asisitiza dhamira ya Serikali kuwezesha ushiriki wa vijana katika maendeleo

Na Mwaandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imeahidi kuendelea kuweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria itakayowapa vijana fursa pana ya kushiriki na kushirikishwa katika michakato yote ya maendeleo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 12, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”.

Amefafanua kuwa dhana ya Ushiriki wa Vijana katika kujenga uchumi imara, ustawi na maendeleo endelevu inatokana na kuwa vijana ndio nguvu kazi, vijana ni kundi kubwa ukilinganisha makundi mengine ya kijamii, vijana ni wabunifu, vijana ni wavumbuzi na vijana ni wadadisi. 

Baadhi ya Vijana wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

“Vijana ni watu wenye mawazo mapya, Vijana ndio chachu ya mabadiliko yenye tija ya Kisayansi na Kiteknolojia na Vijana ndio warithi na waendelezaji wa historia na falsafa ya Mataifa yao,” amesema Prof. Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako amesisitiza kuwa kiwango cha ushiriki wa vijana kwenye shughuli za kiuchumi na za kijamii kwa ajili ya ujenzi wa Taifa hapa nchini kipo kwa asilimia 80.

“Matokeo ya utafiti wa nguvu kazi ya Taifa ya Mwaka 2020/21 yanaonesha kuwa, idadi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 inakadiriwa kufikia watu Milioni 18.3. Kati yao, vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa maana ya economically active population ni Milioni 14.6,” amesema Prof. Ndalichako.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa kati ya watu Bilioni 8 Duniani kote, Idadi ya Vijana ni Bilioni 1.8.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu imeratibu Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, Vijana Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walitekeleza masuala mbali mabli kama vile; Kongamano la Kitaifa na shughuli za kujitolea kwenye  usafi wa mazingira katika fukwe za bahari na Bonanza la Michezo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akiangalia sehemu ya bidhaa za wadau wa masuala ya Vijana walioshiriki kwenye  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

Wazo la kuwa na Siku ya Vijana Kimataifa lilitolewa na vijana kwenye Mkutano wa Vijana wa Dunia (World Youth Forum) uliofanyika Mjini Vienna nchini AustraliaMwaka 1991 

Kuanzia Agosti 12, 2000 nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles