27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana nchini wahimizwa kujiajiri

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Vijana wa jumuiya Afrika Mashariki wametakiwa kutumia uzoefu walionao ili kuweza kujiajiri wenyewe badala ya ukisubiri kuajiriwa na Serikali.

Akizungumza leo Agosti 12, 2022 jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, Balozi wa Vijana Afrika Mashariki, Jesca Mshama amesema changamoto kubwa kwa vijana ni ukosefu wa ajira.

Amesema lengo kubwa la siku ya vijana ni kuwasaidia kuweza kupata fursa za kiuchumi zitakazoweza kuwasaidia kujikwamua.

“Leo tupo hapa kuweza kuwasaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwapatia fursa zinakazowaletea maendeleo,” amesema Jesca.

Ameongeza kuwa asilimia 6 ya vijana Duniani wanaaminikuwa bado sauti zao hazijasikika.

Aidha, amefafanua kuwa asilimia 52 ya vijana ndio wanaoweza kuchagua viongozi na shughuli zozote za kimaendeleo kuweza kushiriki kwa sababu wanaamini wanasikilizwa na viongozi.

Katika hatua nyingine Jesca amewataka viongozi wa Serikali kuangalia vijana kwa jicho la kipekee katika kuondoa mifumo kandamizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles