22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Muhongo amshukuru Rais Samia kwa mradi wa maji

Na Shomari Binda,Musoma

Mbunge wa Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mradi mkubwa wa maji jimboni humo.

Akitoa shukrani hizo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa maji wa Mugango-Kiabakari hadi Butiama wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 70 unakwenda kumtua ndoo mama kichwani, Prof. Muhongo amesema kuwa unaendakuondoa kilio cha maji kwa wananchi wa msoma vijijini.

Aidha, Prof. Muhongo amesema lipo eneo la Bugwema ambalo likitumika kwa kilimo cha umwagiliaji litainufaisha taifa katika suala la chakula.

“Tunakushukuru sana mheshimiwa Rais kwa mradi huu mkubwa wa maji ambao unakwenda kumtua mama ndoo kichwani na kutusaidia kiuchumi, katika jimbo letu tuna vijiji 68 ambavyo vyote vina miradi ya maji ambayo inasimamiwa vizuri na Ruwasa na tunaamini itakamilika,” amesema Prof. Muhongo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi, amesema Serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 120 kwa miradi ya maji na kuishukuru kwa kazi kubwa inayofanya.

Waziri wa maji, Jumaa Aweso, amesema wizara itasimamia mradi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati na wananchi wanautumia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles