29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Kata ya Ilala yaridhishwa ujenzi madarasa ya Uviko

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ilala kimesema kimeridhishwa na ujenzi wa vyumba 17 vya madarasa yanayotokana na fedha za Uviko – 19 yaliyojengwa katika Shule za Sekondari Mivinjeni na Msimbazi zilizopo kwenye kata hiyo.

Akizungumza wakati wa kukagua vyumba hivyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ilala, Habibu Nasser, amezipongeza shule hizo kwa usimamizi mzuri wa fedha hizo.

“Sisi ni watekelezaji wa ilani tumeona ni vyema katika kusherehekea miaka 45 ya CCM tuje tukague madarasa yaliyojengwa kwa fedha za Uviko – 19. Tumeyaona na tumeridhika, tunawapongeza wote kwa usimamizi mzuri wa fedha na kuyajenga kwa ubora,” amesema Nasser.

Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Saad Khimj, amesema madarasa hayo yatamaliza changamoto ya wanafunzi kurundikana darasani na kuboresha ufundishaji.

Khimj ambaye pia ni Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam amesema wametenga Sh milioni 45 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mivinjeni na kwamba kati ya fedha hizo Sh milioni 25 zitatoka halmashauri na Sh milioni 20 zitatolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala kupitia mfuko wa jimbo.

Aidha amesema wanaendelea kushughulikia changamoto zingine za shule hiyo ikiwemo ya upungufu wa viti na meza za walimu pamoja na madawati na kwamba baada ya muda mfupi zitakwisha na watoto watasoma katika mazingira mazuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi, Pantaleo Maghali, amesema walipokea Sh milioni 140 za ujenzi wa vyumba saba na kwamba tayari vimekamilika na kuanza kutumika.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Mivinjeni, Imani Kundema, amesema walipokea Sh milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 ikiwemo chumba cha maabara na kwamba vyote vimekamilika na tayari vimeanza kutumika.

Amesema ujenzi wa vyumba hivyo umeongeza idadi ya wanaunzi wa kidato cha kwanza ambapo mpaka sasa tayari wamepokea wanafunzi 235.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles