27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Pompeo: Tutaweka vikwazo kwa mauaji ya Khashoggi

new york, marekani

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Mike Pompeo, amesema huenda itachukua wiki kadhaa, kabla ya nchi hiyo kupata ushahidi wa kutosha kuwawekea vikwazo washukiwa waliohusika katika mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashogi.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, mauaji ya Khashoggi yamesababisha uhusiano mbovu na ushirikiano duni kati ya Marekani na Saudi Arabia.

Aidha, taarifa hizo zimeeleza kuwa, mauaji ya Khashoggi yamechagua jina la mrithi wa Mfalme Mohamed bin Salman.

“Tunaendelea kutafakari kuwawekea vikwazo watu ambao tumefaulu kuwatambua hadi sasa kuwa walihusika katika mauaji hayo. Tutahitaji labda wiki kadhaa kabla ya kupata ushahidi kamili ili kufanikisha vikwazo hivi, lakini ninafikiri tutafikia hapo,” amesema Pompeo.

Awali, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani alisema mauaji hayo yanakiuka sheria za kimataifa.

Pompeo amesema Marekani ina uhusiano wa kimkakati na Saudi Arabia na wana nia ya kuhakikisha kwamba uhusiano huo hauharibiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles