24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Brazil kuhamishia ubalozi wake Jerusalem

rio de janeiro, brazil

RAIS mteule wa Brazil, Jair Bolsonaro, ametangaza kuwa nchi yake itaiga mfano wa Marekani kwa kuhamisha ubalozi wao ulioko  nchini Israel kutoka mjini Tel Aviv kwenda Jerusalem nchini humo.

Bolsonaro amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, ambapo amefichua kuwa wanapanga kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem, akiongeza kuwa, Israel ni taifa huru na wanaheshimu hilo.

Marekani iliuhamisha ubalozi wake Israel kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem mnamo Mei mwaka huu, hatua iliyowaghadhabisha Wapalestina na viongozi wakuu wa Kiislamu.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amelikaribisha tangazo hilo kwa mikono miwili.

Netanyahu, akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, amempongeza Bolsonaro kwa nia yake akisema ni ya kihistoria, iliyo sawa na inayopendeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles