27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

POMBE YA MALWAA NA UNYWAJI WAKE

malwaa

NA SIDI MGUMIA, TIIRA, UGANDA

Kama walivyo waafrika wengine, Waganda nao wamekamilika kwa mila, desturi na utamaduni wao. Na tukiongelea hilo, ubunifu wa kutengeneza pombe za kienyeji, ni miongoni mwa tunu za utamaduni huo wa Waganda.

Waganda hao ambao wanapatikana katika kijiji cha Tiira wilayani Busia nchini Uganda, wanatengeneza aina nyingi za pombe za kienyeji ikiwemo Malwaa na huzinywa kwa namna za kipekee.

Pombe ya Malwaa ni ile inayotengenzwa kwa mtama huku ikichanganywa na malighafi nyingine na huwa na ladha ya uchachu ambao ndio haswa kivutio katika pombe hiyo kwa mujibu wa watumiaji.

Bei yake ni shilingi 600 za kiganda kwa lita ambayo ni sawa na shilingi 400 ya Tanzania. Na kwa bei hiyo pengine ndiyo maana wengi wanaipenda kwani hata mtu yeyote wa kipato cha chini anaweza kuinunua.

Hata hivyo, Serekali ya kijiji hicho hairuhusu watu kuuza pombe au kunywa nyakati za mchana ikiwa ni moja ya namna yakuwafanya wanakijiji hao wafanye kazi kwa bidii ili kujipatia kipato lakini pia kuleta maendeleo katika kijiji chao kwa ujumla.

Kwasababu hiyo basi, wanakijiji hulazimika kuanza kuburudika na pombe hiyo jioni mara baada ya kumaliza shughuli zao za kila siku ambapo wengi wao ni wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu lakini wapo pia wakulima.

Zaidi ya hapo, kinachofurahisha katika unywaji wa pombe hiyo ni yale matumizi ya mirija ambapo watu zaidi ya 20 ambao ni wake kwa waume huuzunguka mtungi huku wakifyonza pombe kwa wakati mmoja.

Katika mazungumzo yakutaka kujua zaidi juu ya starehe yao hiyo, bwana mmoja aliyetambulika kwa jina la Japhet Koip (45) alisema huwa wanafarijika sana wanapokunywa kutoka katmtungi mmoja na kwa siku huwa wanakunywa mitungi zaidi ya minne ambayo ina ujazo wa lita zaidi ya kumi.

Koip anasema ni pombe kali na chachu sana lakini hicho ndicho haswa kinachowavutia katika pombe hiyo, huku akisisitiza kuwa kukosa kuinywa ni kuikosa raha ya dunia.

Ni kweli ni starehe lakini ifahamike kuwa matumizi ya pombe kupita kiasi ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuzuilika ambayo husababisha vifo vingi kote duniani.

Utafiti mmoja unahusisha pombe na kila kifo 1 katika 25 kote duniani na kwamba 5% ya miaka wanayoishi watu na ulemavu hutokana na matumizi ya pombe pia kuleta magonjwa kama kisukari, kansa ya utumbo, ini na mengine mengi.

Vilevile, kwa hesabu za kila siku, mwezi na hata mwaka wanakijii hawa hutumia kiasi kikubwa cha fedha kununulia pombe hiyo, na kwa mwaka na kwa tafsiri ya kawaida tu, pesa hiyo wangeiweka kwenye maswala ya msingi kama vile elimu, afya, miundo mbinu na mengineyo, Tiira ingekuwa mbali sana kimaendeleo sasa ukizingatia kuwa wamejaaliwa kuwa na madini mengi ya dhahabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles