27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WATANZANIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUIOMBEA NCHI AMANI

mkesha

Mkesha wa dua maalum ya kitaifa ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Desemba 31 katika mikoa zaidi ya 10 umepangwa kufanyika tena mwaka huu.

Akizungumzia mkesha huo, Mwenyekiti wa mkesha huo mkubwa wa kitaifa, Askofu Godfrey Emanuel amesema kuwa katika maombi hayo wataimboea nchi amani na utulivu.

Pamoja na hilo Askofu Emanuel amasema watamuombea pia Rais John Magufuli katika majukumu yake makubwa ya kuiongoza nchi.

Mkesha huo utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam ambapo dua hiyo itafanyikia Uwanja wa Taifa, Songea, Singida, Iringa, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Musoma, Lindi lakini pia Zanzibar.

Askofu Emanuel amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi  ili kuimbea nchi amani na Baraka tele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles