27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

UKOSEFU WA VYANZO VYA MAJI VYAKUELEWEKA BADO NI CHANGAMOTO

maji

Na Sidi Mgumia, Tororo, Uganda

Ni ukweli usiopingika kwamba, huduma za kijamii kama vile maji, bado ni changamoto zinaendelea kuisumbua Afrika kila uchao.

Kutokana na ukosefu wa vyanzo vyakueleweka vya maji, watu haswa wa maeneo ya vijijini hutaabika sana kwa adha hiyo.

Inasikitisha sana katika karne hii ya 21 bado kuna watu katika nchi nyingi barani Afrika, wanachangia maji na wanyama.  Mama anachota maji hapa na ng’ombe au punda anakunywa maji pale.

Hii maana yake ni kwamba Changamoto ya upatikanaji wa maji safi inaendelea kuwepo pamoja na uwekezaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya mataifa, hali iko hivyo Tanzania lakini Uganda pia wanakutana na changamoto hiyo hiyo.

Katika kijiji cha Aburiye A wilayani Tororo, Uganda wananchi hulazimika kuamka alfajiri kutembea kilomita kadhaa, wake kwa waume na hata watoto kufuata maji tena kwenye chanzo kimoja kinachopatikana katika kijiji hicho.

Kwa mujibu wa wenyeji, hicho ndicho kisima pekee kinachowapatia maji , huku wanawake wakilalamika kushinda zaidi ya saa 6 mpaka 8 wakisubiri kupata maji hali inayopelekea kukosa muda wakufanya majukumu yao mengine ya siku kwa wakati.

Madhara ya swala hilo ni makubwa ambapo kwa muda mwingi ambao watu wanasubiri foleni ili wachote maji, vijana hutumia mwanya huo kuwarubuni watoto wa kike na kufanya vitendo vya ngono, matokeo yake wasichana wengi hupata mimba zisizotarajiwa na kuharibu maisha yao kwa ujumla.

Grace Asio ambaye ni mkazi wa kijiji hicho anasmea kwa ujumla ni kwamba licha ya kuwa wote wanataabika na janga hilo bado wanawake na watoto ndio wanaoumia sana kwani wao ndio kundi linalotegemewa kuchota maji na kwa bahati mbaya hulazimika kwenda umbali mrefu kutokana na kuwa kuna chanzo kimoja tu katika eneo hilo.

Na hili huzidi kuwa baya zaidi kadri ya msimu wa ukame katika vijiji hivyo unavyozidi kushamiri ndivyo umbali wa kuyafuata maji kwa matumizi unaendelea kuongezeka.

Hata hivyo, kwa upande wa Tanzania, suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti ya mwaka na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali usiozidi mita 400.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles