22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YAUNDA MADAWATI TISA KUPAMBANA UKATILI

kamanda-wa-polisi-ilala

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala limefungua madawati tisa katika vituo vikubwa vya polisi na vya kati kwa ajili ya kuwahudumia wanawake na watoto wanaonyanyaswa kijinsia.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema wameandaa maandamano ya amani yatakayoanzia Tazara kuelekea Vingunguti katika Viwanja vya Shule ya Msingi Vingunguti na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

Pia alisema katika kupambana na ukatili wa jinsia, wameanzisha madawati katika ofisi ya RPC Ilala, Wilaya ya Kati, Kariakoo, Stakishari, Buguruni, Pangani, Tabata, Salenda Bridge na Vingunguti.

Alisema makosa mengi yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo yote na alitoa mfano kuwa mwaka jana kesi 633 za unyanyasaji wa jinsia na ukatili ziliripotiwa na kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu kesi 1,094 zimeripotiwa.

Alisema kesi hizo zimeripotiwa baada ya kupata taarifa za siri kutoka kwa raia wema na kwa upande wa migogoro ya ndoa wametoa rufaa kwenda manispaa kitengo cha ustawi wa jamii.

Kwa mwaka jana, alisema jumla ya kesi 52 zilipewa rufaa na mwaka huu kesi 70 zilipewa rufaa.

“Makosa ya jinai yaliyojitokeza kila wakati ni kulawiti, kubaka, vipigo, shambulio la aibu, shambulio la kudhuru mwili, lugha ya matusi na shambulio la kawaida, kesi hizo ziko katika hatua mbalimbali.

“Zingine ziko kwa mwanasheria, zingine mahakamani na upelelezi wa kesi nyingine hazina muendelezo baada ya jamii kuripoti na kutotokea kuendelea na kesi hizo,” alisema Hamduni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles