24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YAMSHIKILIA ALIYEDAI ANA UWEZO KUMFUFUA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo
NA HARRIETH MANDARI - GEITA

JESHI la Polisi Mkoa wa Geita, linamshikilia mkazi wa Katoro, Hapiness John (22), kwa kusababisha vurugu baada ya kutoa taarifa kuwa ana uwezo wa kumfufua aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Juma Charles (25), aliyefariki Novemba, mwaka jana.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema Januari 3, mwaka huu, saa nne asubuhi, katika Mtaa wa Bugayambilele ambako mtuhumiwa ni mpangaji wa mama wa marehemu, alidai kuwa Charles hajafariki dunia na kwamba amewekwa msukule na jirani yake, Rebeca Lusana (mama Ratifa) ambaye ni fundi cherehani mtaani hapo.

“Mwanafunzi huyo alikufa kwa ajali ya gari na alizikwa pembeni ya nyumba yao na vurugu ilianza baada ya mtuhumiwa aliyekutwa akiwa anamwaga inayosadikiwa kuwa ni dawa za kienyeji huku akitoa maneno yasiyoeleweka kwenye uwanja wa nyumbani kwa marehemu huyo,” alisema Mwabulambo.

Alisema baada ya mtuhumiwa kuwahakikishia ndugu kuwa Charles yuko hai na anatembea mtaani kila siku, walimshika mtuhumiwa na kumshinikiza awapeleke alipo ili wakamchukue jambo lililozusha vurugu na umati wa watu kujaa eneo hilo.

Gazeti hili lilishuhudia umati wa wakazi wa mji huo waliofurika katika eneo hilo kushuhudia marehemu aliyekuwa akisubiriwa kufufuliwa, huku wengine wakiwa na mawe makubwa mkononi kwa nia ya kumpiga mtuhumiwa hali iliyosababisha polisi kuwatawanya.

Kamanda Mwabulambo, alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi hadi uchunguzi utakapokamilika na akikutwa na hatia atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuwa na nia ya kuvunja amani na kutoa taarifa ya uongo.

Akisimulia mkasa mzima, mama wa marehemu, Rebeca Salumu, aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio alikuwa anajiandaa kusafiri kwenda Bariadi na alipokuwa akitoka nje, alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa ananyunyizia dawa nje ya uwanja wa nyumba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles