25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

“Polisi wameturejeshea amani iliyotoweka sababu ya ‘Panya Road'”

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wahanga wa matukio ya uhalifu yaliyofanywa na vijana wanaojiita ‘Panya Road’ wamelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kuimarisha hali ya amani kwenye maeneo pamoja na kuliomba jeshi hilo kupitia, IGP. Camillius Wambura kuendeleza na Operesheni za kukabiliana na wahalifu ikiwemo majambazi na wahalifu hasa Panya Road kwa ajili usalama wao.

Mwenyekiti wa Mtaa Majengo Vingunguti, Chande Mohammed Msoke.

Wito huo umetolewa leo Jumapili Oktoba 2, 2022 wakati wahanga hao ambao ni wakazi wa Vingunguti Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam walipozungumza na vyombo vya habari kuhusiana na matukio ya kiuhalifu yaliyofanywa na Panya Road sambamba na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi ambapo wamesema kwasasa amani imerejea.

Akizungumza kwa Uchungu, Aisha Rajabu ambaye mtoto wake aliyejulikana kwa jina Kinahe Baraka alifariki kwa kuchomwa kisu na Panya Road amelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali za kisheria wahalifu wote kwa manufaa ya wananchi.

“Wamemuua binti yangu Kinahe Rajabu alikua ananisaidia, anajituma sana katika kazi zake, kama wao Panya Road wanauwa watu kwanini wao wasiuawe, tunaliomba Jeshi la Polisi litusaidie kukabiliana nao, maana wakiwaaha watatumaliza wote,” amesema Aisha.

Kwa upande wake Mzee Christopher John ambaye mtoto wake ni moja ya Panya Road waliokamatwa na Jeshi la Polisi amesema yeye kama mzazi anaumia mtoto wake kujihusisha na uhalifu na ukizingatia amemuonya zaidi ya mara moja.

Christopher John,

“Mimi mtoto wangu ni Panya Road na sasa amekamatwa na Jeshi la Polisi kama mzazi naumia sana kwa sababu nilishamuonya na kuna wakati nilitamani hata nimnywe supu kwa sababu ya tabia yake mbaya” Amesema Christopher John (Baba Mzazi wa Panya Road)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Majengo Vingunguti, Chande Mohammed Msoke amesema tangu Jeshi la Polisi lifanye Operesheni ya kuwakamata Wahalifu (Panya Road) kwa sasa hali ni shwari na wanatembea muda wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles