27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

GF Truck yapongezwa kwa kusaidia uchangiaji damu salama Geita

Na Anna Ruhasha Geita

Kampuni inayouza magari makubwa ya mizigo pamoja na mitambo mbalimbali ya ujenzi ya GF Trucks & Equipment imewezesha upatikanaji wa chupa za damu salama 25 kwa ajili kuunga mkono uchangiaji wa damu nchini ili kuokoa uhai wa wagonjwa wenye uhitaji wa mkoani Geita.

Wananchi wakiendelea na uchangiaji damu salama mkoani Geita.

Hayo yameelezwa na Meneja Masoko na Mahusiano Kampuni ya GF Trucks, Smart Deus wakati Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko kutembelea banda hilo katika maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayoendelea mkoani Geita.

“Mhe. Waziri GF Trucks tunaadhimisha miaka 15 tangu tumeanza kutoa huduma kwa jamii na katika maonesho haya tumedhamini upatikanaji wa damu salama chupa 25, lakini pia kwa wateja watakaonunua bidhaa kwetu katika maonesho tutawafanyia huduma(service) bure mteja yeye ataweza kununua vipuri,“ amesema Deus.

Aidha, Muuguzi Kitengo cha damu salama katika Hospitali ya Mkoa wa Geita, Angelina Swai ameishukuru GF Truck kwa kudhamini chakula na vinywaji kwa vikundi vya wasanii na Bodaboda waliojitokeza kuchangia jumla ya chupa 25 za damu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa damu salama mkoani humo.

“Mh Waziri nikukalibishe katika banda letu la kuchangia damu salama lakini pia nitumie nafasi hii kuishukuru kampuni ya GF Trucks ambayo imewezesha kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa chupa hizi za damu, hata hivyo tangu maonesho ya teknolojia ya madini yameanza hapa mkoani kwetu zaidi ya chupa za damu salama 148 zimepatika,” amesema Swai.

Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko akizungumza katika na waandishi wa Habri alipotembelea banda la kampuni ya GF Truck.

Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko ameipongeza kampuni ya GF Truck kwa uzalendo wake katika jamii kwa kutumia maonesho hayo kuwezesha upatikanaji wa damu salama, huku akiziomba kampuni zilizopo katika maonesho hayo kuiga kwa GF Trucks kusaidi uchangiaji wa damu salama ili kuokoa maisha ya watu.

“Ni wapongeze sana GF Truck na msichoke kuisaidia jamii kwa mambo mbalimbali hususan jamii ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini ili sekta hii iweze kukua na kuchangia pato la taifa,“ amesema amesema Waziri Biteko.

Kampuni hiyo ya GF Truck mbali na kuwezesha uchangiaji damu salama katika maonesho hayo, wao pia ni moja ya wafadhili wakubwa wa maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji yanayoendelea mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles